ads1
Nafasi za kazi Tume ya Taifaya Uchaguzi Kusimamia Uchaguzi 2025
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Nafasi hizo ni kwa ajili ya Tanzania Bara na Zanzibar, zikihusisha Mratibu wa Uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya, na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo.
Recommended:
Kwa mujibu wa tangazo la Tume, Mratibu wa Uchaguzi atakuwa na jukumu la kuratibu habari na taarifa za uchaguzi, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa, na kuwa kiunganishi kati ya Tume na wadau wa uchaguzi katika maeneo husika. Nafasi hii inapatikana Unguja na Pemba.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya atasimamia shughuli za uchaguzi katika wilaya yake, kuhakikisha utunzaji wa vifaa na matumizi sahihi ya fedha za uchaguzi, pamoja na kutoa taarifa za maendeleo kwa mujibu wa maelekezo ya Tume.
Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania, watumishi wa umma, na kuwa na shahada au stashahada ya juu katika fani yoyote. Aidha, hawapaswi kuwa viongozi wa vyama vya siasa au kuwa na rekodi ya makosa ya kinidhamu au jinai. Maombi yanapokelewa kuanzia Aprili 3 hadi Aprili 23, 2025.
Read Also:
Read Also:
ads2