New Vacancies at Jeshi la Polisi

ads1

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne wenye sifa zifuatazo: –

SIFA ZA MUOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
  • Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
  • Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.
  • Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
  • Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I-
  • Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Points) 26 hadi 28.

Recommended:

 
  • Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
  • Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
  • Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8″) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4″) kwa wanawake.
  • Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
  • Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha.
  • Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
  • Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.
  • Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
  • Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
  • Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
  • Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
  • Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
  • Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
  • Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili.

Read Also:

Nafasi za kazi Jeshi laPolisi March 2025

FANI ZINAZOTAKIWA KWA KILA NGAZI YA ELIMU TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.


 




BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI 



ads2